Description
Wasifu Wa Mwandishi:
Erin Ensinger alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Cairn na Chuo Kikuu cha Arcadia akiwa na shahada za Biblia, kazi ya kijamii, na Kiingereza. Alifanya kazi kama mfanyakazi wa kijamii, profesa wa Kiingereza, na mwandishi wa habari kwa miaka kadhaa. Kwa sasa anawasomesha watoto wake nyumbani na anahudumu kama mhariri mkuu wa Authenticity Book House.
Muhtasari wa Kitabu:
Je, huwa unauangalia ulimwengu wetu na kujiuliza, “Nini kilienda vibaya? Kwa nini mambo mabaya huwapata watu wema? Je, ninaweza kupata tumaini?”
Tunaishi katika ulimwengu uliojaa hadithi za kusikitisha. Kitabu cha Tumaini katika Ulimwengu Wenye Huzuni kinasimulia hadithi za watu wanne walioteseka na manyanyaso, kuachwa, na kuondokewa na wapendwa wao. Maumivu yao yaliwasukuma kukata tamaa hadi injili, au “hadithi njema,” kuhusu Yesu ilipowapa tumaini.
Yesu aliandika mwisho mpya wa hadithi zetu zote za kusikitisha alipokufa kwa ajili ya dhambi zetu na akafufuka tena. Wewe, pia, unaweza kupata amani na kusudi katika maisha haya na kutumaini ulimwengu bora ujao ambapo Yesu anatuahidi kwamba hatutakuwa na huzuni tena. Fungua tu kitabu hiki ili usome hadithi pekee inayoweza kubadilisha maisha yako milele.







